Takwimu kuhusu utafiti wa UNICEF OGIP
- Nchi Zinazoshiriki
- 21
- Jumla ya Wajibu
- 22,043
Tovuti ndogo ya UNICEF na ripoti
Kuhusu Mradi wa Utoto Unaobadilika
Motisha
Tunaishi katika enzi ya mabadiliko ya haraka na makubwa. Kadiri ulimwengu unavyobadilika — kuwa wa kidijitali zaidi, wenye utandawazi zaidi, na anuwai zaidi — utoto unabadilika nao. Mradi wa Utoto Unaobadilika — ushirikiano kati ya UNICEF na Gallub — uliundwa ili kuchunguza mabadiliko haya, na kuelewa vyema zaidi inachomaanisha kuwa mtoto katika Karne ya 21. Mradi huu unanuia kujibu maswali mawili: Kukua leo kuko vipi? Na vijana wanaona ulimwengu kwa utofauti kwa njia ipi? Ili kujibu maswali haya, tulitaka kusikia kutoka kwa watoto na vijana wenyewe. Kulinganisha uzoefu na mitazamo ya vijana dhidi ya watu wenye umri mkubwa hutoa mwelekeo thabiti wa kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika, na mahali ambapo vizazi hutofautiana na kuungana. Lengo kuu la mradi ni kuwafanya vijana kuwa sehemu muhimu— uzoefu wao na matarajio — katika kazi ya kuboresha maisha ya watoto wote, leo na katika siku zijazo.
Utafiti
Ili kuchunguza maswali na mada za Mradi, UNICEF na Gallup zilibuni utafiti maalumu, uliotekelezwa katika nchi 21 kote duniani. Ikipata ustadi wake kutoka kwa kufanya Kura yake ya Moani ya Dunia ya kila mwaka, Gallap ilichunguza sampuli wakilishi za angalau watu 1,000 katika kila nchi (1,500 huko India). Katika kila nchi, sampuli iligawanywa katika vikundi viwili vya umri: wenye umri wa miaka 15 hadi 24 (kulingana na ufafanuzi wa Umoja wa Mataifa wa vijana), na wale wenye umri wa miaka 40 na zaidi. Utafiti ulifanywa kati ya Februari na Juni 2021. Wajibu wote walifikiwa kwa simu. Iliyoundwa kwa usaidizi wa wataalamu anuwai, zana ya utafiti inajumuisha maswali ambayo yalikuwa yamefanyiwa majaribio katika kura nyingine za maoni, pamoja na mapya yaliyobuniwa hasa kwa ajili ya Mradi wa Utoto Unaobadilika. Maelezo zaidi kuhusu methodolojia yanaweza kupatikana hapa.
Tovuti ndogo
Tovuti hii ndogo ilitolewa na UNICEF ili kuwawezesha watu kutoka duniani kote, hasa watoto na vijana, kuangazia maswali ya Mradi na kuchunguza matokeo yake. Tunatumai itakufurahisa! Tovuti hii ndogo ilitengenezwa na kampuni ya kusanifu, CLEVER°FRANKE. Hakuna data kuhusu watumiaji inayokusanywa kupitia kwa tovuti hii ndogo.
Matokeo
Matokeo yaliyowasilishwa katika tovuti hii ndogo yanatokana na data ya utafiti moja kwa moja. Marejeleo yote ya idadi ya jumla au wastani—kama vile, “kwa wastani” au “wastani wa”—yanarejelea matokeo ya utafiti kwa swali lililotolewa kwa nchi ya wastani miongoni mwa zote 21 zilizofanyiwa utafiti. Vilevile "wastani" wa kikundi cha mapato cha nchi husika hutokana na matokeo ya utafiti kutoka kwa nchi ya wastani katika kikundi hicho cha nchi. Ukizingatia ukubwa wa sampuli za nchi, na mgawanyiko wa sampuli katika vikundi viwili vya umri, matokeo mengi yanayowasilishwa kwenye tovuti hii ndogo yana nafasi ya makosa ya takribani pointi +/- 4 za asilimia katika kiwango cha imani cha 95%. Nafasi za makosa zitakuwa kubwa zaidi kwa vikundi vidogo vilivyo ndani ya idadi ya watu. Maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufafanua matokeo yanaweza kupatikana katika ukurasa wa methodolojia hapa.
Jifunze zaidi
Ugunduzi wa kina zaidi wa matokeo ya Mradi unaweza kupatikana katika ripoti ya Mradi, ambayo inapatikana kwa Kiingereza, Kifaransa, Kihispania na Kiarabu. Watumiaji wanaotaka kuchambua zaidi wanahimizwa kukagua hojaji, methodolojia, data ndogo kamili na kijitabu cha misimbo kilichounganishwa kwenye ukurasa huu. Ikiwa una maswali yoyote, au ungependa kutwambia jinsi unavyotumia Mradi, tafadhali tutumie barua pepe kwa Changing-Childhood@unicef.org.
Rudi kwenye utangulizi