Teknolojia ya Kidijitali

Nafasi za mtandaoni

Ni ulimwengu wa kidijitali. Kizazi chako kimeunganishwa vipi?

Tulifanya utafiti miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15-24 na 40+ katika nchi 21 ili kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika.

Soma zaidi kuhusu utafiti
Umekuwa mtandaoni mara ngapi katika mwezi uliopita, iwe unaangalia barua pepe, kuvinjari, au kwenda kwenye mitandao ya jamii?

Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.

Rudi kwenye swali
Utafiti wetu ulitambua kuwa kwa wastani, 77% ya vijana huingia mtandaoni kila siku.
Hao ni wengi mno zaidi ya wale walio na umri wa miaka 40+, ambao ni nusu yao tu wanaotumia mtandao kila siku.
Lakini si kila mtu ameunganishwa. Kuna mgawanyiko mkubwa wa kidijitali kote ulimwenguni…
Watu wenye umri wa miaka 14-24 wanaosema huwa wanaingia mtandaoni kila siku100%
Zimbabwe15%Japani96%
0%
Ndani ya Japani, 96% kati ya vijana huingia mtandaoni kila siku.
Lakini ndani ya Zimbabwe, ni 15% pekee hufanya hivyo.
Zana za kidijitali na huduma za mtandaoni zinaweza kunufaisha watoto kwa njia mbalimbali.
Je, unafikiri ni faida gani kubwa ya watoto kuwa mtandaoni?

Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.

Rudi kwenye swali
Kwa wastani, idadi kubwa ya vijana wanasema watoto hunufaika sana kutoka kwa kuwa mtandaoni katika sehemu hizi:
Kujuana,
kuwa wabunifu,
…na kujifurahisha.
Zaidi ya yote, vijana wana uwezekano mkubwa wa kuripoti elimu kama faida kubwa ya watoto kuwa mtandaoni.
Watu walio na zaidi ya miaka 40 pia wanasema mtandao unaweza kuwanufaisha watoto sana, lakini wana shauku ndogo kuliko vijana. Hilo ni kweli kuhusu:
Kujuana,
kuwa wabunifu,
kujifurahisha,
na elimu.

Iwapo kila mtoto duniani angekuwa mtandaoni, hili lingeendeleza kubuni nafasi sawa kwa wote kwa kiwango kipi?

Shiriki hadithi hii

Jifunze zaidi kuhusu kipengele hiki cha jinsi utoto unavyobadilika

Teknolojia ya kidijitaliHatari za mtandaoni