Mabadiliko ya Tabia ya Nchi

Hatua ya tabia ya nchi

Uharibifu unaosababishwa na mzozo wa tabia ya nchi unatuzingira. Baadhi ya serikali, kampuni na watu binafsi wanaongeza juhudi za kupunguza athari zake. Je, zitatosha?

Tulifanya utafiti miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15-24 na 40+ katika nchi 21 ili kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika.

Soma zaidi kuhusu utafiti
Unafikiri wanadamu wanaweza kupunguza athari nyingi za mabadiliko ya tabia ya nchi?

Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.

Rudi kwenye swali
Kwa wastani, idadi kubwa ya 86% ya vijana wanaamini kuwa wanadamu bado wanaweza kuchukua hatua ili kupunguza idadi kubwa ya athari mbaya za mabadiliko ya tabia ya nchi. Wana tumaini!
Unafikiri serikali yako inafaa kuchukua hatua kubwa ili kushughulikia mabadiliko ya tabia ya nchi?

Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.

Rudi kwenye swali
Kwa wastani, 73% ya vijana wanasema kuwa serikali zao zinafaa kuchukua hatua kubwa.
% ya vijana wanaounga mkono hatua shupavu za serikali kwa mabadiliko ya tabia ya nchi
Nchi zenye mapato ya chini/chini ya kati
83%
Nchi zenye mapato ya juu ya kati
66%
Nchi zenye mapato ya juu
70%
Tulipata uungaji mkono mkubwa zaidi miongoni mwa vijana kwa hatua ya serikali kwa mabadiliko ya tabia ya nchi katika nchi maskini.
Hilo linadhirisha mengi kwani nchi hizi zina uwezo mdogo zaidi wa kukabiliana na mzozo wa tabia ya nchi, lakini bado ziko katika hatari zaidi ya kuathiriwa na matokeo yake.
Kwa kushangaza, hatukupata pengo kubwa la vizazi katika maoni haya: Wazee wana uwezekano sawa wa kuamini kuwa athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabia ya nchi zinaweza kukomeshwa na kwamba hatua shupavu ya serikali inahitajika.
Eneo moja ambapo tuliona mgawanyiko wa vizazi: ikiwa nchi zinapaswa kushirikiana inapokuja kwa kupambana na changamoto kubwa za ulimwengu.
Idadi kubwa ya Watu wenye umri wa miaka 15-24 wanasema kuwa nchi yao ingekuwa salama zaidi ikiwa serikali zao zingeshirikiana na nyingineIdadi kubwa ya watu wenye umri wa miaka 40+ wanasema kuwa nchi yao ingekuwa salama zaidi ikiwa serikali zao zingeshirikiana na nyingine
BangladeshiIndonesiaMaliNaijeriaMarekani
Hapa, vijana wanaunga mkono zaidi serikali za mataifa kushirikiana kuliko kufanya kazi peke yao.
Hili ni kweli hususan ndani ya Indonesia, Marekani, Naijeria, Bangladeshi na Mali.