Mabadiliko ya Tabia ya Nchi
Tatizo lingine la tabia ya nchi
Mabadiliko ya tabia ya nchi husababisha jaribio lisilo la kifani kwa binadamu. Mzingile huu utaathiri kizazi cha vijana kwa njia isiyo sawa. Je, vijana wanaelewa changamoto hiyo vyema kwa kiasi gani?
Tulifanya utafiti miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15-24 na 40+ katika nchi 21 ili kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika.
Soma zaidi kuhusu utafitiJibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliKwa wastani, ni 80% pekee ya vijana wanaosema kuwa wamesikia kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi.
Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliKwa wastani, ni 56% pekee waliochagua ufafanuzi sahihi wa mabadiliko ya tabia ya nchi: kupanda kwa joto la wastani la dunia na matukio mabaya zaidi ya hali ya hewa yanayotokana na shughuli za binadamu.
Waliosalia wanafikiri kwamba mabadiliko ya tabia ya nchi humaanisha mabadiliko ya misimu katika hali ya hewa.
Ni dhahiri kuwa ufahamivu wa mabadiliko ya tabia ya nchi miongoni mwa vijana ulimwenguni haujakamilika hata kidogo.
Hili ni kweli hususan katika nchi maskini.
Kwa wastani, 77% kati ya vijana katika nchi zenye mapato ya juu wanasema kwamba wamesikia kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi na wanaweza kutoa ufafanuzi wake vyema.
Fungu hili ni 23% tu kwa wastani katika nchi zenye mapato ya chini na chini ya kati.
Ukosefu wa uelewa kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi si mzozo unaowaathiri vijana pekee.
Kwa wastani, watu wenye umri mkubwa hawakufanya vyema kwenye maswali haya.
Ukosefu wa kuelewa maana ya mzozo wa tabia ya nchi unamaanisha ukosefu wa uwezo wa kupambana nao. Hiki ni kikwazo kikubwa kwa hatua ya kimataifa yenye ufanisi.