Wakala

Uwezo wa mtoto

Watoto wengi hawana haki yao ya kupiga kura. Lakini wanaweza kufanya maoni yao kusikilizwa kwa njia tofauti. Ni nani anasikiliza?

Tulifanya utafiti miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15-24 na 40+ katika nchi 21 ili kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika.

Soma zaidi kuhusu utafiti
Unafikiri ni muhimu vipi kwa wanasiasa kusikiliza maoni ya watoto wanapofanya maamuzi?

Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.

Rudi kwenye swali

Kwa wastani, idadi kubwa ya vijana wanaamini kuwa ni muhimu sana kwa maoni ya watoto kusikilizwa.

Hilo si jambo la kushangaza. Lakini inaonekana kwamba watu wenye umri mkubwa huwa na mwelekeo wa kukubaliana nao!

% ya watu walio na umri wa miaka 40+ ambao wanaamini kuwa ni muhimu sana kwa viongozi wa kisiasa kuwasikiliza watoto wanapofanya maamuzi
Nchi zenye mapato ya juu
47%
Nchi za Mapato ya Juu ya Kati
67%
Nchi Zenye Mapato ya Chini/Chini ya Kati
60%

Nchi zinazoendelea zina idadi kubwa zaidi ya watu wanaounga mkono viongozi wa kisiasa kuwasikiliza watoto.

Ni jambo la mantiki mno kusikiliza maoni ya watoto katika ulimwengu unaoendelea, ambapo watoto ni fungu kubwa la idadi ya watu.

Katika nchi zenye mapato ya chini na chini ya kati, 48% ya idadi ya watu ni watoto. Kwa wastani, 60% ya watu wenye umri mkubwa wanasema kuwa ni muhimu sana kwa wanasiasa kuwasikiliza watoto katika nchi hizi.

Kwa kulinganisha, katika nchi zenye mapato ya juu, ni 20% pekee ya idadi ya watu ni watoto. Kwa wastani, 47% ya watu wenye umri mkubwa katika nchi hizi wanasema ni muhimu sana kwa wanasiasa kuwasikiliza watoto.

% ya watu walio na umri wa miaka 40+ ambao wanasema kuwa ni muhimu sana kwa wanasiasa kuwasikiliza watoto wanapofanya maamuzi100%
Bangladeshi30%Naijeria94%
0%

Miongoni mwa watu wenye umri mkubwa, tunaona uungaji mkono mkubwa zaidi kwa wanasiasa kuwasikiliza watoto huko Naijeria…

…na Zimbabwe. Katika nchi hizi mbili, nusu ya idadi ya watu ni watoto.

Tunawezaje kuwahimiza wanasiasa kuzingatia zaidi maoni ya vijana?

Shiriki hadithi hii

Jifunze zaidi kuhusu kipengele hiki cha jinsi utoto unavyobadilika

WakalaUhuru wa kuwa mtoto