Utandawazi
Raia wa kimataifa
Ni nani anayejitambulisha zaidi kama raia wa kimataifa?
Shirika la UNICEF pamoja na shirika la Gallup yaliwauliza vijana na watu wazima katika nchi 55 jinsi wanavyoona ulimwengu kwa sasa.
Soma zaidi kuhusu utafitiAsilimia kubwa ya vijana wanasema wanahisi kuunganishwa zaidi na ulimwengu.
Hiyo, kwa sehemu, inaonyesha uwezo mkubwa wa intaneti – ambayo inasaidia kuunganisha watu duniani kote.
Tuliangalia iwapo vijana—ambao hawajawahi kujua ulimwengu bila intaneti—ni walimwengu zaidi kuliko wazee wao.
Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliKinyume na watu wazima, watu wenye umri wa miaka 15 hadi 24 kwa sasa wanajua tu ulimwengu ulioundwa na utandawazi na muunganisho dijitali. Mabadiliko katika ulimwengu mzima huenda yanachochea mabadiliko katika utambulisho.
Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliKauli zote hizi nne—kuishi jijini, kuwa na elimu ya juu, kuwa na uwezo wa kufikia huduma ya intaneti, na kutegemea vyanzo dijitali vya habari—zinasaidia kufafanua hisia za uraia wa kimataifa.