Kuwa na matumaini mema

Mtazamo wa jumla

Je, maisha yetu bora zaidi yamepita au bado yaja? Tazama jinsi maoni yako yanavyolingana na ya watu kote ulimwenguni.

Tulifanya utafiti miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15-24 na 40+ katika nchi 21 ili kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika.

Soma zaidi kuhusu utafiti
Je, unafikiri ulimwengu unazidi kuwa mahali bora au pabaya zaidi kwa kila kizazi?

Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.

Rudi kwenye swali
% ambao wanafikiri kwamba ulimwengu unakuwa
Mahali bora
57%
Mahali pabaya zaidi
34%
Kwa wastani, watatu kati ya vijana watano wanasema kuwa wanafikiri ulimwengu unaelekea kwa mustakabali bora.
% ya vijana ambao wanafikiri kwamba ulimwengu unazidi kuwa mahali bora100%
Mali29%Indonesia82%
0%
Ingawa matumaini mema ni ya kawaida miongoni mwa vijana, kiwango chake hutofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Ni kubwa zaidi ndani ya Indonesia ambapo 82% ya vijana wanaamini kuwa ulimwengu unakuwa mahali bora.
Kwa kulinganisha, ni 29% ya vijana pekee ndani ya Mali walio na mtazamo huu chanya kuhusu ulimwengu wetu.
Unafikiri vijana na watu wenye umri mkubwa wanalingana vipi inapokuja kwa kuwa na matumaini mema, kwa wastani?

Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.

Rudi kwenye swali
Katika zote isipokuwa nchi tatu — India, Moroko, na Naijeria — vijana wanaonyesha matumaini mema kuliko watu wenye umri mkubwa.
Katika baadhi ya nchi, pengo kati ya vizazi ni dhahiri kabisa.
Ndani ya Japani vikundi hivyo viwili vya umri vina maoni tofauti sana kuhusu mafanikio ya ulimwengu.
Hili ni kweli katika takribani Marekani…
…na Ajentina.
Kwa jumla, kwa kila mwaka unaoongezeka kwa umri, watu wana uwezekano mdogo kwa 1% kusema kuwa ulimwengu unakuwa mahali bora.
Mambo mengine kando na umri pia huathiri mitazamo ya watu. Watu wanaoripoti kupata matatizo ya kibinafsi ya kifedha wana uwezekano mdogo wa kuwa na matumaini mema kwa ulimwengu. Aidha, wanawake wana uwezekano mdogo kwa 6% kuliko wanaume kusema kuwa ulimwengu unakuwa mahali bora.