Afya ya Kiakili

Usumbufu wa kiakili

Watu wanahisije nafsini mwao?

Tulifanya utafiti miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15-24 na 40+ katika nchi 21 ili kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika.

Soma zaidi kuhusu utafiti
Tuliuliza vijana na watu wenye umri mkubwa kuhusu ustawi wao wa kiakili. Fanya jaribio la maswali ili kuona walivyojibu.
Kwa wastani, ni fungu lipi la vijana linaripoti kwamba huwa wanahisi dukuduku, kuwa na wahaka au kuwa na wasiwasi sana?

Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.

Rudi kwenye swali
Kwa wastani, ni idadi ndogo tu juu ya theluthi moja ya vijana (36%) wanasema huwa wanahisi dukuduku, kuwa na wahaka au kuwa na wasiwasi mara kwa mara.
Hiyo inalinganishwa na 30% kati ya watu wenye umri mkubwa.
Lakini mgawanyiko wa vizazi kuhusu wasiwasi sio sawa katika nchi zote…
Idadi kubwa ya watu watu walio na umri wa miaka 15-24 wanaripoti kuhisi dukuduku, kuwa na wahaka au kuwa na wasiwasi mara kwa maraIdadi kubwa ya watu walio na umri wa miaka 40+ wanaripoti kuhisi dukuduku, kuwa na wahaka au kuwa na wasiwasi mara kwa mara
Vizazi vya watu wenye umri mdogo vina wasiwasi zaidi ndani ya Marekani…
…Ufaransa…
na Ujerumani.
Wakati vizazi vya watu wenye umri mkubwa vina wasiwasi zaidi ndani ya Lebanoni...
…Ukraine…
na Bangladeshi.
Kwa wastani, ni fungu lipi la vijana linasema kwamba huwa wanahisi msongo wa mawazo au kuwa na ari ndogo ya kufanya mambo mara kwa mara?

Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.

Rudi kwenye swali
Kwa wastani, 19% kati ya vijana wanasema kwamba huwa wanahisi msongo wa mawazo au kuwa na ari ndogo ya kufanya mambo mara kwa mara.
Hiyo inalinganishwa na 15% kati ya vizazi vya watu wenye umri mkubwa.
Usumbufu wa kiakili umeenea zaidi miongoni mwa baadhi ya vijana kuliko wengine.
Unadhani ni sifa ipi kati za zifuatazo inahusishwa na kuhisi dukuduku, kuwa na wahaka au kuwa na wasiwasi mara kwa mara miongoni mwa vijana?

Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.

Rudi kwenye swali
% ya vijana ambao huhisi dukuduku, kuwa na wahaka au wasiwasi mara kwa mara
Vijana walio na umri wa miaka 20-24 wana uwezekano mkubwa wa kuripoti kuwa huwa wanahisi dukuduku, kuwa na wahaka au kuwa na wasiwasi mara kwa mara kuliko wale walio na umri wa miaka 15-19.
% ya vijana ambao huhisi dukuduku, kuwa na wahaka au wasiwasi mara kwa mara
Vijana ambao wamemaliza chuo wana uwezekano mdogo wa kuripoti kuhisi dukuduku, kuwa na wahaka au kuwa na wasiwasi kuliko wale ambao hawajamaliza.
% ya vijana ambao huhisi dukuduku, kuwa na wahaka au wasiwasi mara kwa mara
Wale ambao wanasema kwamba huwa wanakumbana na matatizo ya kifedha wana uwezekano mkubwa wa kuripoti kuwa huwa wanahisi dukuduku, kuwa na wahaka au kuwa na wasiwasi mara kwa mara kuliko wale ambao wanasema kwamba wana fedha za kutosha.
Kuna wasiwasi unaoongezeka kuhusu hali ya afya ya kiakili miongoni mwa vijana duniani kote. Ni dhahiri kuwa wasiwasi huo unastahiki kuwepo.

Unadhani ni nini kinaweza kufanywa ili kuboresha ustawi wa kiakili wa vijana?

Shiriki hadithi hii

Jifunze zaidi kuhusu kipengele hiki cha jinsi utoto unavyobadilika

Afya ya KiakiliKuwa na mkazo