Kuwa na matumaini mema

Mafanikio ya siku zijazo

<0>Wengi wa vijana wanahisi ulimwengu unaendelea kuboreka muda unavyosonga. Je, wanakadiria vipi matazamio ya kiuchumu katika nchi zao kizazi chao kinavyojiandaa kuwa watu wazima?

Tulifanya utafiti miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15-24 na 40+ katika nchi 21 ili kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika.

Soma zaidi kuhusu utafiti
Tuliuliza vijana ikiwa wanafikiri watoto katika nchi yao watakuwa na hali bora au mbaya zaidi ya kiuchumi kuliko wazazi wao watakapokuwa wakubwa.

Unafikiri ni fungu lipi linasema watakuwa bora zaidi?

Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.

Rudi kwenye swali
% ambao wanafikiri kwamba watoto katika nchi yao watakuwa na hali bora ya kiuchumi kuliko wazazi wao
54%
Bora
Kwa wastani, 54% kati ya vijana wanasema kwamba watoto katika nchi yao watakuwa na hali bora ya kiuchumi kuliko wazazi wao watakapokua.
Ni 38% tu waliojibu kwamba watoto watakuwa na hali mbaya zaidi kuliko wazazi wao.
Tena, vijana wana matarajio chanya zaidi kuliko vizazi vyenye umri mkubwa.
Kwa wastani, watu walio na zaidi ya umri wa miaka 40 wana uwezekano mkubwa wa kusema kwamba watoto watakuwa na hali mbaya zaidi ya kiuchumi kuliko wazazi wao.
Jibu hili la matumaini kutoka kwa vijana ni ishara kubwa ya imani kwa maendeleo.
Kulinganisha viwango vya maisha vya mtu na vya wazazi wake ni mojawapo ya vigezo muhimu ambavyo watu hutumia kutathmini mafanikio maishani.
Kwa kipimo hiki, vijana wana imani kubwa kuhusu matazamio ya kizazi chao…
… lakini sio upesi sana!
Imani hii kwa maendeleo miongoni mwa vijana haipatikani katika nchi nyingi tajiri.
Huko, vijana wana uwezekano mara dufu wa kusema kwamba wanatarajia watoto wa siku hizi kuwa na na hali mbaya zaidi ya kiuchumi kuliko wazazi wao, dhidi ya kuwa na hali bora.
Wengi wa vijana katika nchi tajiri wana rasilimali na nafasi ambazo vijana wengi katika nchi zinazoendelea wanatamani mno.
Hata hivyo wanapotazama mustakabali wao, vijana katika nchi tajiri wanalemewa na kuyumbika kwa uchumi.

Tunawezaje kukuza matazamio ya kiuchumi ya vijana katika mustakabali usio dhahiri?

Shiriki hadithi hii

Jifunze zaidi kuhusu kipengele hiki cha jinsi utoto unavyobadilika

Kuwa na matumaini memaMtazamo wa jumla